Guardiola: Nimekuja Man City kuipa taji la Ligi ya Mabingwa

Muktasari:

Licha ya kikosi cha Guardiola kushinda mechi 10 mfululizo kwenye Ligi Kuu ya England hata hivyo wachambuzi wa soka wanaeleza kwamba bado ni mapema kuipa ubingwa.

England. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema wakati anapewa kibarua Manchester City miongoni mwa vipengele kwenye mkataba wake vilieleza ni lazima aipe Manchester City taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Licha ya kikosi cha Guardiola kushinda mechi 10 mfululizo kwenye Ligi Kuu ya England hata hivyo wachambuzi wa soka wanaeleza kwamba bado ni mapema kuipa ubingwa. Hata hivyo jambo hilo limeipa nguvu City kufanya vyema kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Manchester City ni timu ambayo inatajwa kufika mbali msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa pamoja na Barcelona, Real Madrid na PSG.
Kikosi hicho cha City leo Jumanne kitashuka dimbani kuonyeshana kazi na Napoli mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani kutokana nna timu hizo kufanya vyema kwa sasa kwenye Ligi zao za nyumbani.