‘Rooney asingepata namba kikosi cha Ujerumani’

Tuesday November 19 2013

WAKATI matumaini ya Waingereza kutwaa Kombe la Dunia mwakani yakilala kwa Wayne Rooney, kiungo wa Chelsea, Andre Schurrle,  ameibuka na kudai kwamba nyota huyo asingepata namba katika kikosi cha sasa cha Ujerumani.

England na Ujerumani zinaingia uwanjani leo Jumanne kucheza mechi ya kirafiki ikiwa ni mwendelezo wa upinzani mkali baina yao na tayari Schurrle ameanzisha vita ya maneno kwa kuichimba timu ya taifa ya Ujerumani.

“Rooney ni mchezaji mzuri, lakini tuna wachezaji wenye ubora sana,  katika kila nafasi tuna wachezaji wawili wenye ubora. Sijui kama angeweza kucheza,” alisema nyota huyo mpya wa Chelsea. Hata hivyo, baadaye Schurrle alituma maoni yake katika mtandao  binafsi wa mawasiliano wa Twitter akisema: “Hilo si nililomaanisha kuhusu Rooney, ni mchezaji mkubwa.”