Zlatan huyo atimkia LA Galaxy

London, England. Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic yuko mbioni kujiunga na miamba ya Marekani, LA Galaxy baada ya kuondoka Manchester United.

Ibrahimovic amefunga mabao 29, katika mechi 53, alizocheza Man United, ambayo amekubali kuvunja nayo mkataba kabla ya kumalizika  mwisho wa msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa Sweden mwenye miaka 36, amecheza mechi saba tu tangu alipoumia mguu wake Aprili mwaka jana.

"Ni muda wa kuondoka baada ya misimu miwili ya mafanikio Manchester United," aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

"Jambo zuri limefikia mwisho. Asante kwa klabu na mashabiki, wachezaji na makocha na viongozi wote waliokuwa pamoja name katika kutegeneza historia yangu hapa."

Ibrahimovic alijiunga na miamba hiyo ya England akitokea Paris St-German mwaka 2016.