Zlatan Simba wa Man Utd

Muktasari:

  • Mchezaji huyo ambaye alivaa jezi namba 10 alionyesha soka la kutakata nyuma ya Romelu Lukaku.

Zlatan Ibrahimovic amejiita simba! Hiyo ni baada ya kutoka katika maumivu na kufanya vizuri na kikosi chake kilichoibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Newcastle jana Jumamosi.

Mchezaji huyo ambaye alivaa jezi namba 10 alionyesha soka la kutakata nyuma ya Romelu Lukaku.

"Nilishawaambia kwamba simba hawaponi kama binadamu wa kawaida, nimezungumza na nimethibitisha hilo.”  Lakini watu wakifahamu aina ya tatizo lililonikabili wanaweza wasiamini kuona moto wangu. Nadhani maumivu yangu ni siri yangu, sina sababu ya kuiambia dunia.

“Nimefurahi kurudi, nimefurahi kuona watu wakiimba jina langu wakati nikipasha. Hilo linanipa nguvu nyingi. Hilo linanifanya nijitume zaidi ninapokuwa uwanjani.

"Wamenionyesha kunijali, najivunia kuwa na mashabiki wa aina hiyo. Kwa kweli nilipata nguvu ya ajabu kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa.

"Nilikuwa na maumivu makubwa, lakini sikukata kukata tamaa. Nilijua ningekaa sawa na kurudi kupambana. Napenda kutimiza malengo. Ninapoamua kufanya jambo fulani huwa nakuwa makini.”