Zlatan, Pogba waitangazia vity Man City

Muktasari:

Wachezaji hao wamepoma majeraha yao na kurejea kikosini wiki hii

London, England. Nyota wa Manchester United, Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic wamekula viapo cha kuhakikisha ubingwa wa ligi na mataji mengine yote, yatatua Old Trafford msimu huu.

Wachezaji hao Pogba na Ibrahimov wamerejea kikosi mwishoni mwa wiki baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Kurejea kwa nyota hao umeisaidia Man United kushinda mabao 4-1 dhidi ya Newcastle United Jumamosi iliyopita.

“Muhimu msimu bado mrefu sana. Kama siamini kuhusu kubeba ubingwa, ni bora niache kucheza mpira. Kama siamini tutabeba taji la ligi msimu huu, ni bora nikaacha kucheza. Nitavua viatu vyangu na kuacna kucheza mpira kabisa. Naamini katika mapambano,” alisema Pogba.

Wakati hilo likisemwa na Pogba, Ibrahimovich naye amesema hivi: “Nadhani tunaweza kuishika Man City, kwanini isiwezekane? Sote tupo hapa kwa sababu tunataka kushinda na tunatambua wao wanaongoza.

“Ona kile ambacho Pogba amekileta kwenye timu, ukichanganya na uzoefu wangu, nadhani kuna uhakika wa kushinda kila kitu. Kama msimu uliopita tulishinda mataji mawili, msimu huu tupo vizuri zaidi. Tunaamini tunachukua ubingwa.”

Man City imeiacha Man United kwa pointi katika msimamo wa ligi, lakini kikosi cha Jose Mourinho wanaamini kwamba kurejea kwa wachezaji waliokuwa majeruhi, Pogba, Ibrahimovic na Marcos Rojo kutawafanya kuwa imara zaidi na kutamba mechi zijazo.