Zigo la lawama lamwangukia Morata Chelsea kufungwa na Bayern Munich

Muktasari:

  • Morata aliyecheza winga ya kushoto ya ushambuliaji alishirikiana vyema na Michy Batshuayi mshambuliaji wa kati.

Mshambulaji mpya wa Chelsea ameangushiwa zigo la lawama baada ya klabu yake kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Bayern Munich kwenye mchezo wa kirafiki alioingia akitokea benchi kabla ya dakika 27 za mchezo kumalizika nchini Singapore.

Morata aliyecheza winga ya kushoto ya ushambuliaji alishirikiana vyema na Michy Batshuayi mshambuliaji wa kati.

Mchezaji huyo aliisaidia Chelsea kupata bao  bada ya kumtengenezea pasi Batshuayi. Hata hivyo Morata hakufunga bao kwenye mechi hiyo ya kirafiki.