Zidane afikiria ubingwa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Kiev. Kikosi cha Real Madrid kimetua Kiev,Ukraine kuikabili Liverpool kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa kesho Jumamosi.

Kocha Zinedine Zidane ametua Ukraine akiwa na wazo moja la kutetea taji lake la ubingwa na kulichukua kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Liverpool wanatambua kwamba iwapo watafanikiwa kutwaa taji hilo msimu huu, watakuwa wameibuka mashujaa mbele ya wapinzani wao Real Madrid.