Zanzibar yapokonywa uanachama Caf

Muktasari:

Rais wa Caf, Ahmad Ahmad aliliambia kamati ya utendaji ya shirikisho hilo iliyoketi jijini Rabat, Morocco leo kuwa Zanzibar haikupaswa kupewa uanachama wa Caf kwa sababu haitambuliki kama nchi.

Dar es Salaam. Kamati ya utendaji ya shirikisho la soka Afrika (Caf) imeipokonya Zanzibar uanachama kutokana na kukiukwa kwa taratibu katika mchakato wa kuipatia haki hiyo.

Rais wa Caf, Ahmad Ahmad aliliambia kamati ya utendaji ya shirikisho hilo iliyoketi jijini Rabat, Morocco leo kuwa Zanzibar haikupaswa kupewa uanachama wa Caf kwa sababu haitambuliki kama nchi.

"Walipewa uanachama pasipo kuangalia muongozo ambao upo wazi. Caf haiwezi kutoa uanachama kwa vyama viwili ambavyo viko ndani ya nchi moja. 

Maana ya nchi inatoka kwenye umoja wa Afrika (UN)  na Umoja wa Mataifa (AU)." alisema Ahmad akinukuliwa na BBC.