Zanzibar Heroes yakomaa na Chalenji

Muktasari:

  • Zanzibar Heroes imepangwa Kundi A katika mashindano hayo pamoja na timu za Tanzania Bara 'Kilimanjaro', Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.

TIMU  ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Cecafa Chalenji yanayotarajiwa kufanyika Desembe 3, mwaka huu nchini Kenya.

Kikosi hicho ambacho kipo chini ya kocha, Hemed Morocco,  kimeweka kambi katika Hotel ya Zanzibar Paradise International iliyopo Amaan Mjini Unguja.

"Tunaamini kuwa michezo ni ushindani, hivyo kwa upande wetu tunaendelea kujipanga vizuri kimchezo ili kuona tunafikia lengo katika mashindano ya Chalenji mwaka huu," alisema Morocco.

Zanzibar Heroes imepangwa Kundi A katika mashindano hayo pamoja na timu za Tanzania Bara 'Kilimanjaro', Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.

Wachezaji walioingia kambini sambamba na kuanza mazoezi ni pamoja na makipa, Ahmed Ali 'Salula'

(Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman 'Wawesha' (JKU), Nassor Mrisho (Okapi), walinzi

Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed 'Sangula' (Jang'ombe Boys), Abubakar Ame 'Luiz'

(Mlandege), Issa Haidar 'Mwalala' (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).

Viungo Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Hamad Mshamata (Chuoni), Omar Juma 'Zimbwe' (Chipukizi) na Mbarouk

Marshed (Super Falcon), Suleiman Kassim 'Seleembe' (Majimaji), Mohammed Issa 'Banka' (Mtibwa

Sugar) pamoja na washambuliaji Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa

'Rais' (Jang'ombe Boys), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto) pamoja na Mwalimu Mohd (Jamhuri).

Hata hivyo, bado kikosi hicho kinawasubiria wachezaji kutoka Tanzania Bara, ambao ni Abdallah Haji

'Ninja' (Yanga), Adeyum Saleh 'Machupa' (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abdulla Kheir

'Sebo' (Azam), viungo Mudathir Yahya (Singida United), Matteo Anton (Yanga) na Seif Rashid

Abdallah 'Karihe' (Lipuli).