Z’bar Heroes yajificha hoteli ya kifahari

Muktasari:

>>Timu hiyo ya visiwani inasaka taji lake la pili la Kombe la Chalenji mwaka huu

Zanzibar. Timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ imeingia kambini kujiandaa na mashindano ya Cecafa Chalenj yanayotarajiwa kufanyika Desembe 3, nchini Kenya.

Kikosi hicho kipo chini ya kocha Hemed Morocco kimeweka kambi yake katika Hotel ya Zanzibar Paradise International Hotel iliyopo Amaan Mjini Unguja.

Heroes imepangwa Kundi A pamoja na Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.

“Tunaamini michezo ni ushindani hivyo kwa upande wetu tunaendelea kujipanga vema kimchezo ili kuona tunafanya vema katika mashindano ya Chalenji mwaka huu,” alisema Morocco.

Miongoni mwa wachezaji walioingia kambi  na kipa Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU), Nassor Mrisho (Okapi).

Mabeki Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula"(Jang'ombe Boys), Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).

Viungo Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Hamad Mshamata (Chuoni), Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi) na Mbarouk Marshed (Super Falcon), Suleiman Kassim "Selembe" (Majimaji), Mohammed Issa "Banka" (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto) pamoja na Mwalimu Mohd (Jamhuri)
Hata hivyo bado kikosi hicho kinawasubiria wachezaji kutoka timu za Tanzania bara ambao hawajajumuika na wenzao akiwamo Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam), Viungo Mudathir Yahya (Singida United), Matteo Anton (Yanga) na Seif Rashid Abdallah “Karihe” (Lipuli).