Yanga yazifungia kazi Singida Utd, Dicha

Muktasari:

Yanga ilitarajiwa kuanza mazoezi juzi Alhamisi,  lakini ilibadili ratiba yake na kuwapa wachezaji wake muda zaidi wa kupumzika  kabla ya kwenda Morogoro kuweka kambi hiyo ya wiki moja.

Dar es Salaam. Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga inayojiandaa na mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Singida United, na ule wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya  Welayta Dicha ya Ethiopia, imeamua kuweka mikakati yake mapema kuzimaliza timu hizo kwa kuweka kambi mkoani Morogoro.

Yanga ilitarajiwa kuanza mazoezi juzi Alhamisi, lakini ilibadili ratiba yake na kuwapa wachezaji wake muda zaidi wa kupumzika  kabla ya kwenda Morogoro kuweka kambi hiyo ya wiki moja.

Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe alisema wameamua kuweka kambi mkoani Morogoro sehemu ambayo itakuwa tulivu kwao kuweza kufanya maandalizi ya kutosha kuifunga Singida inayonolewa na kocha wa zamani wa timu hiyo, Hans Van Pluijm .