Yanga yatinga makundi, kulamba zaidi ya Sh. 600 mil za CAF

Muktasari:

Katika mchezo wao leo Jumatano uliochezwa katika jiji la Hawassa, Yanga ilifungwa bao hilo dakika ya pili na Mtogo Arafat Djako.

KIKOSI cha Yanga kimesonga mbele hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuindoa Wolaitta Dicha kwa jumla ya mabao 2-1, ikiwa ni baada ya kushinda nyumbani 2-0 na kufungwa ugenini 1-0.

Katika mchezo wao leo Jumatano uliochezwa katika jiji la Hawassa, Yanga ilifungwa bao hilo dakika ya pili na Mtogo Arafat Djako.

Bao hilo la pekee lilitokana na kona iliyokwenda moja kwa moja na kumpita beki wa Yanga, Kelvin Yondani 'Vidic' ambaye alishindwa kuukoa na Djako kuumalizia.

Kutokana na matokeo hayo, Yanga itasonga mbele katika hatua hiyo na itaweka kibindoni kiasi cha zaidi ya  Sh. 600 mil kutoka CAF.

Safari ya Yanga katika hatua hiyo, ilianza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika iliifunga St Louis ya Shelisheli jumla ya mabao 2-1, ikafungwa na Town Ship ya Botswana 2-1 ikadondoshwa kwenye shirikisho.