Yanga yafuta matumaini ya Ndanda FC kuchukua pointi

Muktasari:

Matokeo hayo kwa Yanga yameiletea mwelekeo mpya kwenye mechi zinazofuata, huku wakifikisha pointi 8 sawa na Simba wakizidiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa lakini Wekundu hao wakiwa juu katika msimamo.

Dar es Salaam. Kikosi cha Yanga kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidhi ya Ndanda FC bao pekee lililofungwa dakika ya 34 na mchezaji Ibrahim Ajib mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Matokeo hayo kwa Yanga yameiletea mwelekeo mpya kwenye mechi zinazofuata, huku wakifikisha pointi 8 sawa na Simba wakizidiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa lakini Wekundu hao wakiwa juu katika msimamo.
Matokeo mengine; Prisons imeichapa bila huruma wenyeji Mwadui ya Shinyanga mabao 3-1 huku Mji Njombe wakichomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Majimaji ikiwa ni siku chache baada ya kumtimua kocha wao, Hassan Banyai.