Yanga mwendo wa goli

Muktasari:

“Tulifanyia kazi suala la kutokutengeneza nafasi na tukalimaliza, likajitokeza tatizo jingine la washambuliaji wetu kutokufunga na kukosa nafasi nyingi za wazi,” alisema Nsajigwa ambaye alistaafu kucheza kwa heshima.

YANGA gari limewaka. Kocha Msaidizi wake, Shadrack Nsajingwa ‘Fusso’ amesema wakati wanauanza msimu walikuwa hawatengenezi nafasi nyingi za kufunga, lakini sasa mambo yamejipa.

“Tulifanyia kazi suala la kutokutengeneza nafasi na tukalimaliza, likajitokeza tatizo jingine la washambuliaji wetu kutokufunga na kukosa nafasi nyingi za wazi,” alisema Nsajigwa ambaye alistaafu kucheza kwa heshima.

“Lakini tuliwapa mbinu za kuweza kutumia nafasi hizo na kuanzia mechi hii ya Mbeya City wameweza kufanya yale ambayo tunahitaji kutoka kwao.”

Fusso ambaye enzi za uchezaji wake aling’ara na Prisons, Moro United na kisha Yanga sambamba na katika timu ya taifa, Taifa Stars, aliongeza: “Mwanzoni timu ilikuwa haipati ushindi wa mabao mengi, lakini kwa sasa kikosi chetu kinaanza kufunguka na kupata ushindi mzuri.

“Hivyo ni matarajio yetu tutaendelea hivi hivi kwa mechi zijazo sababu lengo letu ni kutetea ubingwa huu wa Ligi Kuu Bara tulionao.”