Yanga kucheza na timu za mchangani Moro

Morogoro. Yanga itakuwa na mchezo wa kwanza wa kirafiki kesho na moja ya timu tatu ndogo walizoomba kucheza nazo kutoka Morogoro baada ya kukamilisha mazoezi ya pumzi na ufundi.
Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema baada ya siku tano kocha wa timu hiyo ameomba apatiwe mechi ndogo ya kuangalia ubora wa uwanjani kwa wachezaji wake.
Saleh alisema bado wanasubiri majibu kati ya timu tatu walizoomba ambapo jibu kamili la kwamba watacheza na timu ipi watalijua leo jioni.
Mratibu huyo amesema kocha Mwinyi Zahera ametaka mechi hiyo isiwe na timu ya Ligi Kuu akitaka kuanza kuwapima wachezaji wake kwa timu nyepesi.
"Tunarajia kesho tutakuwa na mechi ya kwanza ndogo ya kirafiki ambayo itakuwa ya kwanza tangu tuanze kambi yetu hapa.
"Kocha ametaja kigezo cha timu anayotaka kupambana nayo na hataki timu ya Ligi Kuu kwa kuwa huu ni mchezo wa kwanza sasa jibu la timu ipo tutakutana nayo tutaijua leo jioni."