Yanga ikipangiwa Al Masry mbona safi tu

Dar es Salaam. Yanga inasubiri droo ya kesho Jumatano inayotarajiwa kufanyika Cairo nchini Misri ili kujua itapangiwa na timu gani miongoni mwa vigogo wa Afrika kama Al Masry, Raja Cassablanca, Enyimba na SuperSpot United ya Afrika Kusini.
Yanga imeangukia kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Rollers ya Botswana.

 Droo hiyo itahusisha timu zilizoanguka kutoka Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na timu ambazo bado zipo Kombe la Shirikisho.
Yanga ndiyo timu pekee iliyosalia kuliwakilisha Taifa kwenye mashindano ya kimataifa lakini kubwa zaidi linalosubiriwa ni iwapo watapangiwa na Al Masry.