Yaani hao Njombe hawajalala

Muktasari:

Mabosi wa Benchi la Ufundi la timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu kwa mara ya kwanza, wamechukua maamuzi hayo ili kurekebisha makosa yote yaliyojitokeza kwenye mechi zao 11 zilizopita ambazo hawakufanya vema.

NJOMBE Mji kumbe nao wajanja, kwani licha ya Ligi Kuu Bara kusimama kwa muda kupisha michuano ya Kombe la Chalenji, wenyewe wala hawakulala kwa sababu kambi yao ya mazoezi imeendelea mwanzo mwisho mpaka sasa.

Mabosi wa Benchi la Ufundi la timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu kwa mara ya kwanza, wamechukua maamuzi hayo ili kurekebisha makosa yote yaliyojitokeza kwenye mechi zao 11 zilizopita ambazo hawakufanya vema.

Kocha wa kikosi hicho, Mrage Kabange, alisema wameamua kukijenga upya kikosi chao ili ligi itakapoanza kuwe na mabadiliko kulinganisha na mechi zao za nyuma.

Nyota huyo wa zamani wa Simba, alisema tayari wamewanyakua wachezaji wawili wa kigeni kutoka Rwanda na wengine wawili wazawa kupitia dirisha dogo la usajili, akiamini watawabeba mara ligi itakapoendelea Desemba 29.

Kocha huyo aliwataja wachezaji hao wazawa ni nyota waliokuwa kikosi cha timu ya taifa ya Vijana ya U17 (Serengeti Boys); Nickson Kibabage na Muhsen Malima.

Katika hatua nyingine majirani wa Njombe Mji, Lipuli FC , tayari imemfanikisha kumchukua straika wa Simba Jamal Mnyate ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho, kilichokuwa mwiba kwa Simba na Yanga katika mechi zao za Ligi Kuu.