Winga Unguja Umisseta awaita Simba

Monday June 11 2018

 

By Saddam Sadick


Mwanza. Mshambuliaji wa timu ya Unguja, Ally Hassan amesema kuwa moja ya ndoto yake katika soka ni kuichezea Simba na anamtamani kuwa kama Shiza Kichuya.


Kinda huyo anayesoma kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Bububu, Zanzibar ni kinara wa mabao katika michezo ya Umisseta katika Kundi D, amesema  anafikiri mafanikio yake kimaisha hapo mbeleni yatapitia soka haswa akiichezea  Simba na Taifa Stars.


Hassan tayari ametupia mabao manne kwenye michezo hiyo na kuisaidia timu yake kuongoza kwa pointi 13 baada ya mechi tano.