Wenger kutimkia PSG

Muktasari:

Kumekuwa na taarifa kwamba PSG inamtaka kocha huyo mwenye umri wa miaka 68, ambaye amewaahidi mashabiki wa Arsenal kwamba atatimka katika kambi ya Emirates mwishoni mwa msimu huu. Hata hivyo PSG inamtaka Wenger katika nafasi ya meneja na sikocha.

PARIS, UFARANSA

NYOTA wa zamani wa Ufaransa Christopher Dugarry anaamini kwamba klabu ya PSG ipo mbioni kumnasa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.

Kumekuwa na taarifa kwamba PSG inamtaka kocha huyo mwenye umri wa miaka 68, ambaye amewaahidi mashabiki wa Arsenal kwamba atatimka katika kambi ya Emirates mwishoni mwa msimu huu. Hata hivyo PSG inamtaka Wenger katika nafasi ya meneja na sikocha.

"Naamini Wenger anauwezo mkubwa wa kuongoza. Anaweza kuongoza kwa mafanikio. Ni mtu wakuheshimika, amekuwa na uthabiti, huwa hayumbi kwa urahisi. Kuna watu ambao hawamkubali lakini ukweli ni kwamba ni kiongozi mzuri.

"Ana uelewa mkubwa wa soka, anaweza kuisaidia timu kutoka hatua moja kwenda nyingine kiuongozi. Hata hivyo kama PSG watamtaka itabidi wampe madaraka anayostahili na wala wasiwe na mpango wa kumuingilia kiutendaji.