Wenger avurungwa akimkumbuka Giroud

LONDON, ENGLAND

ARSENE Wenger amesema kimoyomoyo straika Olivier Giroud ni Arsenal na amekwenda Chelsea kwa sababu tu anataka kulinda nafasi yake kwenye kikosi cha Ufaransa ili akacheze fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Russia baadaye mwaka huu.

Fowadi huyo Mfaransa alihama kutoka Emirates kwenda Stamford Bridge kwenye dirisha la Januari kwa dili la Pauni 18 milioni ambapo alisajili mkataba wa miaka mitano na nusu kuitumikia Chelsea.

Giroud alikuwa hapati namba mbele ya Alexandre Lacazette, lakini ujio wa Pierre-Emerick Aubamenya ulimvuruga zaidi na kuona hatakuwa na muda wa kutosha kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi hicho cha Wenger na kuamua kutimkia kwa Antonio Conte.

Wenger alisema fowadi huyo mwenye umri wa miaka 30 hakutaka kabisa kuihama Arsenal na ndiyo timu iliyo moyoni mwake na yupo Chelsea kwa ajili ya kupata nafasi tu ya kwenda Russia kwenye Kombe la Dunia.

"