Waziri Mkuu kushuhudia Dodoma FC na Namungo Jamhuri

Muktasari:

  • Timu hizo mbili zinakutana kwa mara ya pili, awali mwezi Agosti zilicheza wilayani Ruangwa mkoani Lindi katika mechi maalum ya kuzindua Uwanja wa Majaliwa utakaotumiwa na Namungo.

Dodoma. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi wa mchezo kati ya wenyeji Dodoma FC dhidi ya Namungo FC leo Jumapili kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Timu hizo mbili zinakutana kwa mara ya pili, awali mwezi Agosti zilicheza wilayani Ruangwa mkoani Lindi katika mechi maalum ya kuzindua Uwanja wa Majaliwa utakaotumiwa na Namungo.

Katika mchezo huo hautakuwa na kiingilio na maalumu kwa timu ya Dodoma FC kutawatambulisha wachezaji wake kwa wapenzi na mashabiki wa timu.

 Katika hatua nyingine, kuna uwezekano Dodoma FC kulitambulisha rasmi basi lao dogo jipya ambalo wamenunua kwa ajili ya kulitumia msimu ujao wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL).