Waziri Mkuu Majaliwa aipa basi Namungo FC

Muktasari:

Basi hilo ni sehemu ya mchango wa Waziri Mkuu kwa timu hiyo ambayo yeye ni mlezi wake ikiwa inatokea katika jimbo lake la Ruangwa mkoani Lindi.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameikabidhi basi la kusafiria timu ya Namungo FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Basi hilo ni sehemu ya mchango wa Waziri Mkuu kwa timu hiyo ambayo yeye ni mlezi wake ikiwa inatokea katika jimbo lake la Ruangwa mkoani Lindi.

Makabidhiano ya basi hilo, yamefanyika leo jimboni Ruangwa ambapo Waziri Majaliwa aliwakilishwa na katibu wa ofisi yake, Hassan Zidadu.

Namungo ni miongoni mwa timu 24 za Ligi Daraja la Kwanza zitakazopambana kusaka nafasi ya kucheza Ligi Kuu msimu wa 2019/2020