Watoto wa mastaa wenye vijiji instagram

Muktasari:

Binti Tiffah anasemekana kuwa mtoto wa pili mwenye ufuasi mkubwa duniani kwenye Insta akiwa na zaidi ya followers milioni moja. Ukiachana na umaarufu wa wazazi wake, mwenyewe kawa maarufu pia. Kitu hicho kimemwezesha kuvutia dili kadhaa za matangazo ya kampuni ya Vodacom ambayo ni kampuni ya mawasiliano, benki ya NMB, na Pampers

UNAAMBIWA maji hufuata mkondo. Ukiachana na mastaa ambao ni kawaida kuwa na ufuasi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na haswa Instagram, sasa ni bayana kuwa pia ipo idadi kubwa ya watoto wao wanaoonekana kukusanya vijiji vya followers huko huko Insta.

Matokeo yake imekuwa nao kuweza kunasa dili za kimatangazo kama wengi wa wazazi wao. Hawa ndio watoto wa mastaa wanaocheza kwenye ligi moja ya kuwa na ufuasi mkubwa kwenye Instagram

DJ KHALED

Mtoto: Asad Khaled

Insta: 2 milioni

Ndiye mtoto mwenye followers wengi zaidi duniani. Kafanikiwa kupata ufuasi huo kutokana na umaarufu mkubwa wa babake bishop. Baraka za kuwa na followers kibao kwenye Insta yake imemwezesha kupata michongo kadhaa ikiwemo kuwa balozi wa mavazi ya watoto Kids Footlocker na Rookier USA

DIAMOND NA ZARI

Mtoto: Tiffah Dangote

Insta: 1.9 Milioni

Binti Tiffah anasemekana kuwa mtoto wa pili mwenye ufuasi mkubwa duniani kwenye Insta akiwa na zaidi ya followers milioni moja. Ukiachana na umaarufu wa wazazi wake, mwenyewe kawa maarufu pia. Kitu hicho kimemwezesha kuvutia dili kadhaa za matangazo ya kampuni ya Vodacom ambayo ni kampuni ya mawasiliano, benki ya NMB, na Pampers

DIAMOND NA ZARI

Mtoto: Prince Nillan

Insta: 720k

Kama tu mkubwa wake, dogo huyu kapata umaarufu kupitia wazazi wake na ni kati ya watoto wa mastaa wenye followers wengi duniani.

Lakini haiishia hapo, hatua hiyo imemwezesha kuangukia michongo ya nguvu ikiwemo kuteuliwa kuwa balozi wa duka kubwa la mavazi ya watoto kule Dar es Salaam GSM Baby Shop

KANYE WEST NA KIM

Mtoto: North West

Insta: 325k

Ni mtoto wa kistaa lakini hana umaarufu sana kama wazazi wake baba rapa na mama soshiolaiti. Hata hivyo binti huyu anaowafuasi wa kiasi cha haja waliompa mchongo wa kuwa balozi wa fasheni ya watoto.

DJ MOH NA SIZE 8 REBORN

Mtoto: Ladasha Belle Wamboi

Insta: 284k

Ni binti ya mastaa hawa wawili wa showbiz ambao wamefanikiwa kuzivutia dili kibao za kimatangazo kutokana na brandi yao. Ladasha naye kaweza kupata dili za maana kutokana na umaarufu wake kwenye Instagramu aliko na zaidi ya wwafuasi lakini mbili na themanini. Mtoto huyo kasuka dili na kampuni ya Softcare Premium kupromoti bidhaa zake za ‘Pampers’. Mtonyo anaoupata sio wa kubahatisha.

VINCENT KIGOSI Na CHUCHU HANSI

Mtoto: Jaden The Baddest

Insta: 179k

Ni mtoto wa mwigizaji mashuhuri wa Kibongo Vincent Kigosi na mpenziwe Chuchu Hansy.

kapata umaarufu kutokana na mwonekanao wake wa kuvutia kama tu ule wa babake. Jaden ni balozi wa mavazi ya Robby One Kids

JAY Z Na BEYONCE

Mtoto: Blue Ivy

Insta: 144k

Jay Z na mke wake Beyonce wana mamilioni ya followers kwenye akaunti zao ila sio wanao. Kifungua mimba wao Blue Ivy anao wafuasi wasiofikia hata robo ya followers wa babake au mamake.

Hata hivyo, amefanikiwa kuvuta dili akiwa ni balozi wa kampuni ya mavazi ya Capital Clothing

KING KAKA

Mtoto: Gweth

Insta: 15k

Wiki iliyopita siku chache tu baada ya babake kuteuliwa kuwa balozi wa kileo chas Remy Martin, Gweth naye alitangazwa kuwa balozi wa mafuta ya watoto ya Marina Naturals.