Washindi wa mbio za baiskeli kwenda Sauzi

Muktasari:

  • Mashindano hayo ya baiskeli yanatarajia kufanyika Jumamosi kwa waendeshaji baiskeli nyota kutoka mikoa yote ya Tanzania.

Washindi wa watatu wa baiskeli katika Tamasha la Majimaji Selebuka wataenda kushiriki mashindano ya kimataifa nchini Afrika Kusini.

Mashindano hayo ya baiskeli yanatarajia kufanyika Jumamosi kwa waendeshaji baiskeli nyota kutoka mikoa yote ya Tanzania.

Mratibu wa mashindano hayo Judith Mbongoro alisema kuwa zaidi ya waendeshaji baiskeli  50 watashiriki.

Alisema waendeshaji baiskeli, wataendesha  umbali wa kilometa 100 kutoka Mbinga na kumalizika kwenye Uwanja wa Majimaji.

“Msimu wa kwanza 2015-2016  tamasha hili la mbio la baiskeli lilifanywa kwa ufanisi mkubwa  sana, tunaamini kuwa viwango vya ushindani mwaka huu vitakuwa juu zaidi kulinganisha na msimu uliopita,” alisema Judith.

Tamasha la Majimaji Selebuka limeandaa  mashindano ya riadhaa, ngoma za asili, maonyesho ya ujasilamali, madahalo katika shule za sekondari na mbio za baiskeli.