Washambuliaji wanne Yanga kuimaliza Rayon leo

Wednesday May 16 2018

 

Kikosi cha Yanga kimedhamiria kuwapa raha mashabiki wake leo Jumatano watakapokipiga na Rayon Sports ya Rwanda baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mkongo Mwinyi Zahera kuwaanzisha kwa pamoja washambuliaji wanne.

Washambuliaji hao watakaounda kikosi cha wachezaji 11 katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi ni Mzambia Obrey Chirwa, Yusuph Mhiru, Juma Mahadhi na Geofrey Mwashiuya.

Wengine ni mlinda mlango Mcameroon Youth Rostand, mabeki ni Hamis Ramadhan 'Kessy', Gadier Michael, Kelvin Yondan 'Vidic na Andrew Vincent 'Dante', wakati viungo ni Pius Buswita na Mzimbabwe Thaban Kamusoko.

Yanga inacheza mchezo huo wa kundi D, mbali na Rayon timu nyingine ni Gor Mahia ya Kenya na USM Alger ya Algeria.