Wanyama anawakubali hakuna mfano Ngasa, Kaseja

Muktasari:

  • Wanyama aliingia Tanzania Juni 18, na lifanikiwa kutembelea maeneo mengi ya vivutio vilivyopo hapa nchini katika kisiwa cha Mbudya na sehemu nyingine.

 Kiungo wa Tottenham Spurs na Kenya 'Harambee Stars', Victor Wanyama yupo hapa nchini kwa mapumziko.

Wanyama aliingia Tanzania Juni 18, na lifanikiwa kutembelea maeneo mengi ya vivutio vilivyopo hapa nchini katika kisiwa cha Mbudya na sehemu nyingine.

Wanyama alisema kuwa anafuatilia ligi ya Tanzania pindi anapopata nafasi, lakini kuna wachezaji anawajua na kuwasikia kutoka hapa nchini.

"Wachezaji ambao nawajua ni Mrisho Ngassa, Juma Kaseja, pia Mbwana Samatta namjua licha ya kutowahi kuonana kwa macho na huwa namfuatilia," alisema.

"Nitakuwepo katika mechi ya Ndondo Cup kesho kushuhudia kati ya Kauzu Fc dhidi ya Faru Jeuri, na huwa napenda michuano hii kwa sababu nilishawahi kucheza kule kwetu Kenya kabla ya kwenda Ulaya," alisema Wanyama.