Ligi ya Wanawake yanoga kinoma

Muktasari:

Lema alisema tofauti na msimu uliopita, msimu huu mashindano hayo ya yameonyesha kupiga hatua kubwa kutokana na idadi kubwa ya timu kuonekana zimefanya maandalizi ya kutosha ingawa zile zilizopo kundi B ndizo zinaonekana kuimarika zaidi.

Wakati hatua ya makundi ya Ligi Kuu ya Wanawake ikikaribia kumalizika, kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Stars', Edna Lema ametoa tathmini ya hatua hiyo ambayo imeonyesha kusifu ushindani uliopo kwenye kundi B kulinganisha na kundi A.
Lema alisema tofauti na msimu uliopita, msimu huu mashindano hayo ya yameonyesha kupiga hatua kubwa kutokana na idadi kubwa ya timu kuonekana zimefanya maandalizi ya kutosha ingawa zile zilizopo kundi B ndizo zinaonekana kuimarika zaidi.
"Kiukweli mashindano ya msimu huu yamekuwa tofauti na yale ya msimu uliopita kwani sasa hivi timu zimejiandaa na nyingine zimefikia hadi kusajili wachezaji kutoka nje ya nchi hali inayoashiria kwamba kipindi kifupi kijacho, ligi ya wanawake Tanzania itakuwa yenye thamani kubwa.
Hadi hapa tulipofikia ambapo hatua ya makundi inaelekea ukingoni, nadhani kundi B ndilo lenye ushindani zaidi kwa sababu hakuna tofauti kubwa ya ubora baina ya timu na timu na ndio maana unakuta zinafungana mabao machache lakini huko kwenye kundi kuna timu zinafungwa hadi mabao tisa jambo ambalo linaonyesha wazi kwamba ushindani," alisema Lema.