Wakala wa Diego Costa atua China kumuuza kwa Pauni 13 milioni

Muktasari:

  • Wakala Jorge Mendes alifanikiwa kuzungumza na viongozi wa klabu hizo ili kuhakikisha mchezaji huyo anapata timu mojawapo kwenye dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa.

Wakala wa Diego Costa ametua China na kukutana na uongozi wa klabu za Shangai SIPG Tianjin Quanjin  na kujadiliana kuhusu kumpeleka kwa mkopo  wa mchezaji huyo kwenye dirisha dogo la usajili muda ukifika.

Wakala Jorge Mendes alifanikiwa kuzungumza na viongozi wa klabu hizo ili kuhakikisha mchezaji huyo anapata timu mojawapo kwenye dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa.

Costa ameridhia kuuzwa kwa pesa ndogo ya Pauni 13 milioni kuliko kurudi Chelsea ambako tayari ameshagoma kujiunga na kikosi cha timu hiyo msimu mpya wa Ligi Kuu England.