Wagombea Urais TFF waonja joto la jiwe

Saturday August 12 2017

 

Dodoma. Wagombea wa nafasi ya urais wa TFF wameonja joto la jiwe kutokana na maswali ya mitego waliyoulizwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho hilo unaoendelea Dodoma sasa.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli alifungua mlango kwa wagombea nafasi ya Urais kuomba kura na kila mmoja alipewa dakika 5, za kujinadi na kujibu maswali ya wajumbe.                       

Aliyeanza ni Wakili Iman Madega"Nimesukumwa na mambo takribani manne. Jambo la kwanza ni uzoefu wangu. Muda wa kulitumikia shirikisho ninao. Mimi nina uadilifu na nidhamu ya matumizi na mwisho ni kwamba mpira wetu una matatizo kwa sasa.

"Nimesukumwa na mambo takribani manne. Jambo la kwanza ni uzoefu wangu. Muda wa kulitumikia shirikisho ninao. Mimi nina uadilifu na nidhamu ya matumizi na mwisho ni kwamba mpira wetu una matatizo kwa sasa                       

Mjumbe Musa Kisocky amemuuliza swali Madega kuhusiana na tuhuma za kuipendelea Yanga                       

"Sitopendelea klabu yoyote na nitaongoza kwa usawa kwa timu zote," alijibu Madega.                       

Aliyefuatia ni makamu wa rais sasa Wallace Karia

"Nimeamua kugombea kwa sababu Mimi ndiye mgombea mwenye uzoefu wa kutosha kuliko wenzangu. Wajumbe msiache mbachao kwa msala upitao- Karia                       

Anayefuata ni Fredrick Mwakalebela: "Nimekuja leo hii kuwaomba mnipe ridhaa kuwa mtunga Sera badala ya mtendaji. Nitarudisha msingi wa utawala bora.

Mwakalebela hadi sasa ndiye mgombea aliyeulizwa idadi kubwa ya maswali

1. Atasimamia vipi fedha ndani ya shirikisho

2. Anawahakikishia vipi wajumbe kuwa hatoondoka madarakani kabla ya muda wake kumalizika

3. Atasimamia vipi utawala bora

Ambayo yote ameyajibu

Anayefuata sasa ni Ally Mayay ameanza kwa kutoa wasifu wake mrefu alionao wa kielimu na kwenye soka.                       

"Nimeishi kwenye mpira wa miguu na nimepitia katika nyanja zote za soka. Kipaumbele changu cha kwanza ni kuanzisha dira ya maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania.”

Ally Mayay amekatishwa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi                       

Ameulizwa swali kuwa Sputanza ambayo yeye ni mjumbe, imekuwa iliendesha mambo kibabaishaji, akichaguliwa hatoiendesha TFF kwa staili hiyo?

Mayay amelijibu swali hilo.

Pia, Mayay ameulizwa swali ni mikakati ipi ataiweka kuimarisha uhusiano wa mikoa na TFF.

Mayay amejibu hivi "kupitia utafiti tutagundua matatizo yote tuliyonayo na ndio maana kipaumbele cha kwanza ni kuwa na dira.”

Anayefuata ni mgombea Urais, Shija Richard: "Mimi ni mtu ambaye ninaamini katika kanuni, sheria na katiba. Nitaondosha tatizo la muingiliano wa mamlaka."

Nikichaguliwa kuwa Rais, nitawaomba tutengeneze dira ya mpira wa miguu ya kipindi cha miaka 20.

Shija Richard ameulizwa swali, ataje majukumu matano ya nafasi ya Urais                        

Amejibu mmoja ni kuongoza mkutano mkuu wa TFF, pili kuongoza kamati ya utendaji.                       

Hakuendelea kujibu. Pia Shija ameulizwa swali lingine ataje timu alizochezea.

Amejibu kwa kutaje uzoefu wake kwenye soka. Ametaja orodha ya timu alizocheze.

Mgombea wa mwisho aliyeitwa ni Emmanuel Kimbe:"Tunahitaji maendeleo ya soka la vijana, soka la akina mama, waamuzi na viwanja bora.

“Nawaomba kura zenu ili jukumu langu liwe kuhakikisha naleta maendeleo kwenye maeneo niliyoyataja," Kimbe.

Kimbe ameulizwa swali, ataweza vipi kudhibiti suala la Usimba na Uyanga ndani ya TFF.                       

"Nitahakikisha TFF inakuwa taasisi imara kwa sababu ndio itaondoa suala la Usimba na Yanga.

Awali

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli anatoa tangazo kuwa mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais, Steven Ally amejiondoa kuwania nafasi hiyo.

"Jana tulipokea barua kutoka kwa bwana Steven Ally ya kuomba kujiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi lakini tayari jina lake lilishakuwepo kwenye makaratasi ya kupigia kura," alisema Kuuli.