Wachezaji mpira wanawake waweka rekodi ya dunia kwa kucheza soka Mlima Kilimanjaro

Muktasari:

  • Eneo hili lipo umbali wa urefu mita 5731 kutoka usawa wa bahari kwa kawaida hali yake ya hewa kuwa oxygen kidogo na baridi si rahisi kucheza.
  • Katika mchezo waliocheza kulikuwa na timu mbili Volcanic Fc na Glacier Fc na wametoka suluhu mchezo ulichezeshwa na waamuzi wenye beji za Fifa Salma Mukansanga wa Rwanda  na Jonesia Rukyaa wa Tanzania  wakisaidiwa na Vicky Allan na Morag Pirie raia wa Scotland

Kilimanjaro.Wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa 20 jana wameshuka mlima Kilimanjaro baada ya kufanikiwa  kucheza soka kwenye eneo creta na kuweka rekodi ya dunia.

Eneo hili lipo umbali wa urefu mita 5731 kutoka usawa wa bahari kwa kawaida hali yake ya hewa kuwa oxygen kidogo na baridi si rahisi kucheza.

Katika mchezo waliocheza kulikuwa na timu mbili Volcanic Fc na Glacier Fc na wametoka suluhu mchezo ulichezeshwa na waamuzi wenye beji za Fifa Salma Mukansanga wa Rwanda  na Jonesia Rukyaa wa Tanzania  wakisaidiwa na Vicky Allan na Morag Pirie raia wa Scotland

Akizungumza baada kupokea ujumbe wa wachezaji hao waliokuwa wanafikia 60, ambao pia walifika kilele cha mlima huo, Mkurugenzi  wa bodi ya Utalii (TTB), Veronica Mdachi alisema Bodi ya Utalii imefurahishwa sana na tukio hilo.

Alisema anaamini litautangaza mlima Kilimanjaro duniani na kuvutia watalii zaidi kuja Tanzania.

Alisema TTB inaamini kufika nchini wachezaji hao na kupanda mlima Kilimanjaro kutavutia watalii wengi duniani.

Naye mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Betty Loiboki alisema ujio wa wachezaji una faida kubwa katika utalii.

Alisema si jambo rahisi kucheza soka katika eneo la creta na akahimiza watalii wengine kuja nchini na kuweka rekodi za kucheza eneo  hilo.Mratibu wa safari hiyo Erin Blankenship  kutoka marekani alieleza tukio walilofanya ni kubwa na ni rekodi ya dunia mchezo wa soka haujawahi kuchezwa katika eneo lililopo umbali wa Mita 5731 ambapo kuna baridi kali na hewa ndogo ya oxygen

Alisema safari ya kupanda mlima licha ya kufika kileleni eneo la uhuru umewapa sifa ya kipekee kucheza mpira juu ya Mlima huo mrefu barani Afrika.

Awali Afisa habari mwandamizi wa TTB, Geofrey Tengeneza alisema tukio la kuchezwa soka Mlima Kilimanjaro litaongeza watalii kwani limevunja rekodi ya dunia.

Ujumbe wa wachezaji hao ulikuwa na wachezaji 60 kutoka Mataifa 20 yakiwepo matatu ya Afrika ambayo ni Tanzania, Rwanda na Afrika Kusini.