Wachezaji Simba wahesabu noti

Muktasari:

  • Nyota wa Simba wameahidiwa kugawana kiasi cha dola 30,000 (Sh68 milioni) watakazopewa kama zawadi kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya SportPesa Super Cup ama zawadi nyingine yoyote watakayopata.

Nakuru. Baada ya kutinga hatua ya fainali ya mashindano ya SportPesa, wachezaji wa Simba wameanza kutiana jeuri ili kupiga mkwanja wa maana.
Nyota wa Simba wameahidiwa kugawana kiasi cha dola 30,000 (Sh68 milioni) watakazopewa kama zawadi kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya SportPesa Super Cup ama zawadi nyingine yoyote watakayopata.
Mara baada ya kuwaondosha Kakamega Homeboys kwenye nusu fainali kiungo wa Simba, Jonas Mkude alisikika akiwaambia wachezaji wenzake kuwa pesa zimewasogelea sasa.
"Tumeshajihakikishia dola 10,000, sasa tupambane tutwae ubingwa," Mkude aliwaambia wachezaji wenzake.