Wachezaji Njombe wakwepa kupita geti kuu

Wachezaji wa Njombe Mji, wameingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, kwa kutumia geti linalotumiwa na viongozi pamoja na mashabiki badala ya geti kuu kama ilivyozoeleka.

 Wachezaji wa Mbeya City wao waliingia uwanjani kwa kutumia basi lao kupitia geti kuu, huku basi la Njombe Mji aina ya Coaster limeingia likiwa limewabeba viongozi tu.

Hata hivyo haijafahamika sababu za wachezaji wa Njombe Mji kutotumia basi lao na kuamua kuingia kwa miguu.