Yanga washindwe wenyewe Afrika

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Tanzania inashiriki hatua hiyo kwa mara ya pili

Yanga imefuzu kwa mara ya pili kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho na ratiba yake itapangwa kesho habari nje kwao katika hatua hiyo kuna timu nane ambazo  zinashiriki kwa mara ya kwanza pamoja uwepo wa klabu mbili za Afrika Mashariki.

Ratiba hiyo itafanyika kesho, Jumamosi, 21 Aprili 2018, katika makao makuu ya CAF, Cairo, Misri saa 9:00 alasiri.

Kwa mara ya kwanza Cecafa itakuwa na timu tatu katika hatua ya makundi Yanga, huku Gor Mahia ya Kenya na Rayon Sports ya Rwanda zikishiriki kwa mara ya kwanza hatua hiyo ni baada ya Shirikisho la Soka Afrika CAF kuongeza idadi ya timu zinazofuzu kwa hatua ya makundi.

Timu nyingine zinazoshiriki kwa mara ya kwanza ni Aduana ya Ghana, Williamsville ya Ivory Coast, UD Songo ya Msumbiji, El Masry  ya Misri, miamba ya Morocco, RS Berkane zote zimefuzu kucheza kwa mara ya kwanza hatua hiyo.

Pia, hatua hiyo kutashudia mabingwa wa zamani wa Afrika, AS Vita (DR Congo), Raja Club Athletic (Morocco), ASEC Mimosas (Ivory Coast) na Enyimba (Nigeria). CARA (Congo) pia iliwahi kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka 1974, nayo inafuzu kwa mara ya pili. Miamba mingine ni Djoliba ya Mali, USM Alger (Algeria), na El Hilal (Sudan).

Timu zilizofuzu

AS Vita (DR Congo), USM Alger (Algeria), El Masry (Misri), Raja Club Athletic (Morocco), CARA (Congo), El Hilal (Sudan), ASEC Mimosas (Ivory Coast),  Gor Mahia (Kenya), UD Songo (Msumbiji), Enyimba (Nigeria), Aduana (Ghana), Yanga (Tanzania), RS Berkane (Morocco), Williamsville (Ivory Coast), Djoliba (Mali), Rayon Sports (Rwanda)