Vyuma vimekaza Mike Oligi ataka kuihama Liverpool

Wednesday November 8 2017

 

By THOMAS MATIKO

MAISHA yamembamba straika wa Liverpool, Divorck Origi 22, mwanawe nahodha wa zamani na straika matata wa Harambee Stars, Mike Okoth Origi na sasa anataka kuihama klabu hiyo na kuhamia mazima Wolfsburg ya Ujerumani aliko sasa kwa mkopo.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alimuuza Origi (aliyekataa kuichezea Kenya) mwanzoni mwa msimu huu kwenda huko Wolfsburg ili aweze kutoa nafasi kwa kifaa kipya Mohamed Salah ambaye toka awasali amekuwa akiwasha moto uwanjani Anfield.

Kinyume na alivyokuwa akilishwa benchi pale Anfiled huku Ujerumani Origi anapata muda wa kutosha uwanjani na ndio sababu iliyompelekea kudokeza kuwa angelipenda kuikacha Liverpool kabisa.

“Najisihi vizuri sana huku, ni klabu nzuri na kwa kweli nafurahia maisha huku. Nahisi ninaweza kupevusha kiwango changu huku na kwenye soka  lolote laweza kutokea” Origi amenukuliwa na jarida moja la Ujerumani akisema.

Mkurugenzi wa klabu hiyo Olaf Rebbe  mwenyewe pia kakiri kwamba, wangelipenda kumnunua kabisa Origi baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika “Tutajadili kinachowezxa kutokea kabla ya msimu kuisha.

Akiwa ana miaka miwili, Divock tayari katudhihirisha ni fowadi mwenye upekee kwa talant yake aliyojaliwa,” Rebbe alinukuliwa vile vile akikubaliana na hoja za fowadi huyo.