Vita ya Yanga vs Azam FC kuhitimishwa leo Uwanja wa Taifa

Kikosi cha Yanga kimejipanga kuhitimisha safari ya mechi za ligi dhidi ya Azam FC itakayopigwa leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa.
Awali, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wao uliopita, nguvu yao wameelekeza kwenye mchezo dhidi ya Azam FC.
Alisema kinachofuata sasa hivi ni kuhakikisha wanapata matokeo watakapokutana na Azam walau waweze kumaliza ligi wakiwa namba mbili kwenye msimamo wa ligi.
Sare ya Yanga dhidi ya Ruvu imewagandisha nafasi ya tatu huku ikiwalazimu kushinda dhidi ya Azam ili waweze kushika nafasi ya pili, na endapo mechi itamalizika kwa droo, hawatoweza kuwapiku Azam kwenye nafasi hiyo.
Yanga mpaka sasa ina alama 52 wakati wapinzani wao Azam wamejikusanyia pointi 55, hivyo mechi itakayowakutanisha leo Jumatatu kama Yanga atashinda ataishusha Azam na kupanda juu kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga