Vipigo, sare yaacha machungu wazee wa kubeti

Muktasari:

  • Michezo ya kubahatisha imeshika kasi kwa sasa hapa nchini kila mwishoni mwa wiki vijana ujipatia pesa kutokana na ubashiri huo.

Dar es Salaam. Wazee wa kutandika mikeke wamekiona chamoto wikiendi iliyopita baada ya Juventus, Monaco, Borussia Dortmund, Chelsea na Arsenal kupoteza katika mechi zao za Ligi Kuu mbalimbali barani Ulaya.

Wadau mengi wa mchezo wa kubahatisha Betting wameishia kulalama kwa vigogo hao kwenye soka la Ulaya ambao wamewachania mikeka yao.

Machungu yalianza Ijumaa pale  Monaco alipofungwa 3-2 na Lyon kwenye Ligue 1, Jumamosi katika Ligi Kuu England nako Liverpool na Mancheater United  zikatoka sukuhu, kwenye Uwanja wa Selhurst Park Chelsea ilikutana na kipigo cha 2-1 kutoka kwa vibonde, Crystal Palace.

Arsenal ikapotea 2-1 kwa Watford, Italia nako hapakuwa shwari  Juventus alipoteza 2-1 mbele ya Lazio, Roma ikapigwa 1-0 na  SSC Napoli.

Bundesliga nako  hali iliendelea kuwa tete kwa Dortmund kufungwa 3-2 nyumbani na  RasenBallsport Leipzig.

Wakati katika LaLiga miamba  Atletico Madrid na Barcelona ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1.