Vipigo vya Miembeni havijamkatisha tamaa kocha

Muktasari:

  • Kocha huyo anaamini pamoja na kuanza vibaya ligi bado vijana wake wananafasi ya kufanya vizuri katika ligi hiyo

Zanzibar. Pamoja Miembeni City kupokea kipigo vitatu mfululizo katika Ligi Kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja, kocha Mkuu wa timu hiyo Mohamed Seif ‘king’  amesema ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na vijana wake katika michezo yao.

Miembeni City imecheza mechi tatu ikiambulia vipigo kutoka kwa Polisi bao 1-0, ikanyukwa na Mafunzo kwa bao 1-0 kabla ya kutandikwa kwa kipigo kama hicho na mabingwa watetezi timu ya JKU.

 “Unajua ukweli lazima nisema mbali ya vipigo hivyo ila viwango vya wachezaji wangu ni vizuri hasa katika mchezo wa juzi tuliocheza dhidi ya JKU nifurahishwa na uchezaji wetu japo tulifungwa”alisema king.

Alisema kuwa wachezaji wake bado wapo vizuri kimchezo na tayari ameshawapima nini wanahitaji ili kuwa tishio katika michezo yao mengine iliyosalia.

 “Michezo hiyo ambayo tumefungwa, kwangu mimi nasema ilikuwa ni sehemu ya kukiangalia kikosi changu ila naamini bado kipo uzuri ijapokuwa kunahitaji marekebisho kidogo tu ya kiufundi ili kukiongezea nguvu zaidi ya kiushidnani,”alisema king.