Vigogo wa PSG hawana masihara usajili wa Mbappe

Uongozi wa PSG wiki hii umepanga kukutana na mshambuliajiwa Monaco, Kylian Mbappe kuhusu kumsajili kwa dau la Pauni 160 milioni.

Mazungumzo hayo na vigogo wa PSG kwa upande mwingine yatampa ahueni Mbappe kujua hatima yake ya soka msimu huu kutokana na kuhusishwa kuhamia klabu mbalimbali vigogo barani Ulaya.

Mbappe anajua kwamba tayari PSG ilishaweka bayana kupitia kwenye vyombo vya habari kuwa imemtengea dau la mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki.