Video: Washindi wa Tuzo za Ligi Kuu walipuka suti matata

Kamati ya tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara imesifu maboresho yaliyofanyika katika mchakato wa kupata washindi mbalimbali wa tuzo za ligi hiyo msimu 2017/2018 huku washindi wa Tuzo hizo wakitinga suti zao zilizowafanya kuonekana nadhifu.
Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hizo, Alhaji Msafiri Mgoyi alisema kamati imefanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa tuzo za msimu wa 2017/2018 zinakuwa na mabadiliko makubwa tofauti na awamu zilizopita.
" Lengo la tuzo hizi ni kuongeza hamasa na ushindani kwenye ligi hivyo niseme kamati ilihakikisha inaendesha zoezi kwa umakini wa hali ya juu ili kupata washindi sahihi.
Vipo vigezo mbalimbali ambavyo tumeviweka katika kupata washindi lakini kubwa zaidi ni muda ambao muhusika amekuwepo kwenye ligi na mchango alioutoa," alisema Mgoyi.