Video: 'Kigogo' mwingine Yanga ajiuzulu

Muktasari:

Kiongozi huyo amesema, amejiuzulu kwa masikitiko kwa sababu alikuwa na muda mrefu wa kuitumikia timu hiyo.

Dar es Salaam: Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amejiuzulu nafasi yake kutokana na shutuma na kashfa ambazo baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakimpa.
Sanga amefanya maamuzi leo Jumatatu alipozungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea, Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Kiongozi huyo amesema, amejiuzulu kwa masikitiko kwa sababu alikuwa na muda mrefu wa kuitumikia timu hiyo.


"Siku ya Ijumaa niliona picha mbalimbali kwenye mitandao zikieleza shutuma mbalimbali juu yangu ikanibidi kufanya hivyo,"alisema Sanga ambaye alifafanua mbali na shutuma hizo baadhi ya watu hao walihamasisha kwenda nyumbani kwake na mapanga, mashoka na majembe.


Kwa mujibu wa katiba ya Yanga, Sanga alitakiwa kumaliza muda wake wa uongozi mwaka 2020.