Vee Money atema cheche

Muktasari:

Vee Money alisema kila msanii ana nafasi yake katika muziki hivyo iangaliwe ulinganishwaji huo unakuwa wa namna gani na sio kwa ushabiki wa mitandaoni kwani inasababisha bifu na wengine kushuka kimuziki.

MWANADADA anayekimbiza kwenye Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, amewafungukia mashabiki wenye tabia ya kushindanisha wanamuziki katika mitandao ili mmoja aonekane yuko juu kwa madai kuwa siyo kitu kizuri.

Vee Money alisema kila msanii ana nafasi yake katika muziki hivyo iangaliwe ulinganishwaji huo unakuwa wa namna gani na sio kwa ushabiki wa mitandaoni kwani inasababisha bifu na wengine kushuka kimuziki.

“Kuna baadhi ya mashabiki siyo wote, wenye tabia ya kupambanisha wasanii kwenye mitandao kwa sababu wana kitu fulani. Kazi ya muziki ni ngumu kama mnavyoona, sasa tukianza kujadiliana sijui fulani ni fulani tunaweka ugumu kwenye lengo letu la kutengeneza muziki mzuri na kuleta burudani. Mie niwaambie ukweli tu sipendi sana hii tabia ya Watanzania kunishindanisha na wasanii kwenye mitandao yao hiyo,” alisema Vee Money ambaye ameachia albamu yake hivi karibuni.