Vanessa Mdee amchana shabiki wa Jux

Muktasari:

  • Wasanii hao wawili wamewahi kuwa wapenzi na sasa inaelezwa kwamba kila mmoja anaendesha maisha kimpango wake.

 

Msanii Vanessa Mdee ameshindwa kuvumilia maneno ya shabiki kwenye akaunti ya Instagram ya Jux na kuamua kumtolea uvivu juu ya maneno yake ya shombo kwa mpenzi wake wa zamani huyo.

Jux aliweka video akifanya shoo ya pamoja na Vanessa Mdee na moja ya shabiki wa Jux wa kike alianza kumponda Jux kuwa anajipendekeza kwa Vanessa na kwenda mbali zaidi na kusema Vanessa hana haja na yeye na hana kitu cha kumpa.

Kufuatia ujumbe huo Vanessa Mdee alishindwa kuvumilia na kuja kumjibu binti huyo kwa kumweleza kuwa yeye si msemaji wake na kudai amekuwa akitoa maneno machafu kila siku kwenye ukurasa huo wa Jux na kusema huenda akawa anamtaka Jux.