VIDEO: Msuva atua kishujaa, aipa matumaini Yanga Kombe la Shirikisho

MSHAMBULIAJI wa Difaa El Jadida, Saimon Msuva ametua kishujaa, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Morocco mara baada ya kumalizika kwa  Ligi Kuu nchi humo 'Batola Pro'.
Msuva  mwenye mabao 11, amemaliza msimu huo kwa kuwa kinara na upachikaji mabao ndani ya klabu yake huku akiwaacha mbali kwa mabao nyota wa kigeni wanaocheza,  Morocco.
 Difaa ambao  wapo kundi B kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika wamemaliza msimu wa 2017/18  wakiwa  nafasi ya tano Ligi Kuu nchini humo.
Msuva ametua nchini kwa mapumziko ya zaidi ya wiki nne kwa ajili ya kusalimia ndugu jamaa na marafiki kabla ya kurejea tena Morocco.
Msimu wa 62 wa Batola Pro unatarajiwa kuanza mwezi, Agosti mwaka huu lakini Difaa inategemewa kuanza maandalizi yao mapema zaidi  ili kujiandaa na Ligi ya mabingwa Afrika ambayo itaendelea, JulaiSent from Yahoo Mail on Android