VIDEO: Kivumbi Ligi Kuu Bara, watani Simba, Yanga Septemba 30

Muktasari:

  • Mchezo huo wa hisani kati ya Mabingwa wa msimu uliopita wa upande wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kombe la ligi 'FA', utachezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Dar as Salaam. Pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2018/19 , linatarajiwa kufunguliwa  Agosti 18 kwa mchezo wa  hisani kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo wa hisani kati ya Mabingwa wa msimu uliopita wa upande wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kombe la ligi 'FA', utachezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mara baada ya mchezo huo  wa hisani, Agosti 22 ndipo zitakapoanza mbio rasmi za kuwamia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ambao utashirikisha jumla ya timu 20.

Akizungumzia ratiba hiyo,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), Boniface Wambura alisema katika upangaji wa ratiba wamezingatia ushiriki wa klabu za Tanzania katika mashindo ya kimataifa.

"Tumezingatia pia kalenda za FIFA, mashindao ya vijana ya Cecafa na hata Kombe la Mapinduzi," alisema ofisa huyo.

Katika michezo ya mzunguko wa kwanza, Agosti 22  Simba itaanza nyumbani kwa kucheza dhidi ya Tanzania Prisons,Ruvu Shooting dhidi ya Ndanda, Alliance dhidi ya Mbao, Coastal Union wachuana na Lipuli.

Singida United dhidi ya Biashara United,Kagera Sugar dhidi ya Mwadui na michezo ya Agosti 23 itakuwa kati Stand United  dhidi ya African Lyon,JKT Tanzania dhidi ya KMC,Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga na Azam itacheza dhidi ya Mbeya City.

Mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga kwenye mzunguko wa kwanza utachezwa Septemba 30,Uwanja wa taifa.