Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kung’arishwa maandalizi ya Ligi Daraja la Kwanza

Friday August 11 2017

 

By Yohana Challe, Mwananchi ychalle@mwananchi.co.tz

Arusha. Mjumbe wa Bodi ya Ligi, Stephen Mnguto ametaka Uwanja wa Shekh Amri Abeid ufanyiwe ukarabati haraka kabla ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) kuanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao.

Mnguto alisema kuwa uwanja huo unapaswa ufanyiwe ukarabati eneo la kuchezewa pamoja na kuwekewa vivuli sehemu ya kukaa wachezaji wa akiba pamoja na benchi la ufundi ili kuzuia jua litakalokuwa linawaka wakati mchezo ukiendelea.

Aliongeza kuwa hajatoa muda maalumu kwa ajili ya kurekebisha maeneo hayo, bali ametoa wazo kwa watumiaji wa uwanja ikiwa ni moja ya njia ya kufanya uwanja wanaotumia kuwa na sifa za ziada.