Usajili wa Simba haujamshawishi kocha kabisa!

Muktasari:

  • Simba ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, pia wametoa mchezaji bora ambaye ni John Bocco, mfungaji bora, Emmanuel Okwi na kipa bora, Aishi Manula.

Dar es Salaam. Aliyekuwa kocha wa Majimaji ya Songea, Habibu Kondo, amesema anashangazwa na usajili unaofanywa na Simba na akawaambia, hautawasaidia kabisa kwenye mashindano yao ya kimataifa ambapo wao ndiyo wawakilisha wa Tanzania Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kondo amesema, Simba ina mashindano ya kimataifa, walipaswa kuangalia zaidi wachezaji ambao watawasaidia katika michuano hayo mikubwa Afrika.

Wanachotakiwa kufanya ni kusawazisha makosa yote waliyoyafanya awali kwani ndiyo mwaka wao wa mabadiriko.

Amesema, Simba imefanikiwa katika mshindano ya ndani na sasa waweka nguvu zao huko na kuwa mfano. 

"Simba na Yanga wanafanya vizuri kwenye Ligi ya Tanzania na wameshachukua makombe zaidi ya 10 kila moja, sasa wabadilike na akili zao ziwaze kimataifa ambako bado hawafanyi vizuri kutokana na maandalizi," alisema.

"Wachezaji wengi waliowasajili sasa, wanaweza mpira wa ndani lakini bado hawawezi kuwapa changamoto wale walicheza hapo msimu uliopita viwango vyao ni vya kawaida.

"Angalia mtu kama Salamba (Adam) anamweka vipi nje, Emmanuel Okwi au John Bocco ni ngumu, wanatakiwa kuangalia zaidi nje ya nchi kupata wachezaji wenye uwezo wa juu na wataweka changamoto," alisema.