Usain Bolt hatihati kushiriki mashindano ya Riadha Dunia London

Muktasari:

Mwanariadha huyo alisema kwa takriban wiki mbili alikuwepo nchini Ujerumani  ambako alikuwa akitibiwa kutokana na matatizo ya mgongo, lakini atajumuika na wapenzi wa riadha kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya Herculis, Monaco nchini Ufaransa.

Ufaransa. Mwanariadha Usain Bolt amesema kutokana na matatizo ya mgongo aliyonayo, atatangaza hivi karibuni iwapo atashiriki  mashindano ya Riadha ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika hivi mwezi ujao London, Uingereza.

Mwanariadha huyo alisema kwa takriban wiki mbili alikuwepo nchini Ujerumani  ambako alikuwa akitibiwa kutokana na matatizo ya mgongo, lakini atajumuika na wapenzi wa riadha kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya Herculis, Monaco nchini Ufaransa.

Mashindano ya Ligi ya Daimond yanatambulika na Shirikisho la Riadha la Duniani (IAAF) nchini humo.

Mashindano hayo huwakutanisha vijana mbalimbali na kuibua vipaji ambapo pia wanariadha maaraufu nchini humo kama vile  Wayde van Niekerk, Maria Lasitskene, Renaud Lavillenie na Caster Semenya watashiriki.