Uongozi wa Liverpool wampa rungu Klopp kumsajili Aubameyang

Muktasari:

  • Aubameyang pia anatakiwa na Paris Saint-Germain na Dortmund wapo tayari kuuza baada ya kuibuka kwa Ousmane Dembele katika safu yake ya ushambuliaji.

Mkurungezi wa Liverpool, Peter Moore amefunga njia kidogo ya klabu hiyo katika kuisaka saini ya mshambuliaji Borussia Dortmund,Pierre-Emerick Aubameyang.

Liverpool ni miongoni mwa klabu zinazowania kuipata saini ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon.

Dortmund inakarisha ofa kwa timu inayomtaka Aubameyang kwa gharama ya pauni61.5 milioni msimu huu.

Aubameyang pia anatakiwa na Paris Saint-Germain na Dortmund wapo tayari kuuza baada ya kuibuka kwa Ousmane Dembele katika safu yake ya ushambuliaji.

Aubameyang ni mfungaji bora wa Bundesliga msimu uliopita akiwa amefunga mabao 31, katika mechi 32.

Dau la pauni 63 milioni haliwezi kuwa tatizo kwa kocha Jurgen Klopp anayetaka kujenga safu yake ya ushambuliaji hasa baada ya kumsajili Mohamed Salah.

Moore amesema hakuna tatizo katika kufanikisha usajili huo.

"Tunahitaji kufanya usajili kwa umakini kwa kupata mkataba bora kwa pande zote katika dirisha hili la usajili.

Aubameyang amekuwa na rekodi nzuri ya ufungaji tangu alipokuwa Ufaransa na klabu ya St Etienne, nyota huyo amefunga mabao 120 katika mechi 189 alizocheza Dortmund tangu aliponunuliwa na kocha wa sasa wa Liverpool , Klopp mwaka 2013.