Unaikumbuka ile michango ya Jangwani?

Muktasari:

Amesema Kamati ya Utendaji ya timu hiyo, inakutana kujadili namna ya watakavyoboresha njia ya kuwafikia mashabiki wao na kuwafanya kuwa na moyo wa kujitolea.

KATIBU wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema wanaboresha mchakato waliouanzisha wa kuwachangisha pesa wanachama kwa lengo la kuongeza kipato cha kufanikisha malengo ya klabu.

Amesema Kamati ya Utendaji ya timu hiyo, inakutana kujadili namna ya watakavyoboresha njia ya kuwafikia mashabiki wao na kuwafanya kuwa na moyo wa kujitolea.

“Unapozungumzia Yanga, ina matajiri, ina wenye kipato cha kati na wasionacho pia, uhamasishaji ukitolewa naamini tunaweza kuwa na hatua nyingine, ukichanganya na zile fedha za wadhamini tutafika mbali,”alisema Mkwasa aliyewahi kuicheza Yanga na baadaye kuinoa pia.

Kuhusiana na maandalizi ya mechi zilizopo mbele yao wakianza na ya leo dhidi ya Ndanda, alisema wapo fiti lakini amesisitiza wachezaji kujituma kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao.