Ngorongoro, Serengeti Heroes zafanya kweli kimataifa

Muktasari:

  • Mabao ya Serengeti yamefungwa na Alphonce Msanga akipiga mawili dakika ya 4 na 59, Mustapha Naukuku dakika ya 27, Edson Mshirakandi ya 28, Japhary Mtoo ya 78 na Kelvin Paul dakika ya 83.

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 'Ngorongoro Heroes' kimeing'oa DR Congo kwa jumla ya penalti 6-5 huku Serengeti Boys nayo ikiichapa Sudan kwa mabao 6-0 na kutinga raundi ya pili ya mashindano hayo yanayoendelea nchini Burundi.

Ngorongoro inayofundishwa na kocha, Ammy Ninje imesonga mbele hatua hiyo baada ya kutoka suluhu  nyumbani jijini Dar es Salaam kisha kulazimisha suluhu kama hiyo katika mchezo wa marudiano uliochezwa leo Jumapili nchini DR Congo.

Kwa matokeo hayo, Ngorongoro Heroes itakutana  na Mali na ikishinda itakutana na mshindi kati ya Cameroon au Uganda katika kuwania kufuzu kucheza fainali hizo nchini Niger, mwakani.

Kwa upande wa kikosi cha Serengeti Boys, kimepita hatua hiyo na kuendelea kuwakilisha nchi.

Mabao yamefungwa na Alphonce Msanga akipiga mawili dakika ya 4 na 59, Mustapha Naukuku dakika ya 27, Edson Mshirakandi ya 28, Japhary Mtoo ya 78 na Kelvin Paul dakika ya 83.